MAAJABU YA PILIPILI KUTENGENEZA MABOMU YA MACHOZI

FLORA HARRISON NA JENNY CHILLERY

Unaweza kustaajabu namna ambavyo mahitaji ya pilipili kuzidi kuwa muhimu kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu,katika hali ya kawaida ni ngumu kuamini kama pilipili ina faida lukuki kwa mwanadamu ukiachilia mbali na matumizi yake kama kiungo kwenye chakula.

Mmea wa pilipili asili yake ni asia na kwa hapa nchini, zinalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar. Nchini India zao hili hutumiwa na hulimwa kwa wingi .

Nchi zenye hali ya joto zaidi hutumia pilipili zaidi kulinganisha na nchi zenye baridi, pilipili hutumika kama kiungo cha mapishi mbalimbali ambapo humea katika maeneo yenye joto 24 hadi 26 na kwenye maeneo ya mwambao.

Zao hilo linahitaji udongo wenye rutuba na unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5 . Mahitaji ya mvua ni milimita 1500 hadi 2000 kwa mwaka,pilipili hukomaa katika miezi tisa hadi kumi ambapo uvunaji wake ni kwa mizunguko mitano hadi sita katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa upande wa pilipili mtama , inaweza juvunwa kwa misimu miwili ya mavuno kwa wastani wa tani 0.35 hadi 3.75 kwa hekta, pilipili zinkua tayari kuvunwa siku 60 hadi 95 kutegemeana na aina ya mbegu iliyotumika,lakini changamoto kubwa katika uvunaji wa pilipili ni keikali iitwayo ‘’Capsaicinoids’’ ambayoinaweza kuwasha kwenye ngozi au macho.

Pia zina harufu kali na zinaweza kusababisha chafya , kupata mafua, kuwashwa kwa pua au macho lakini kwenye chakula hufanya kiwe na radha ya kuvutia kwa mlaji.kuna aina mbalimbali za pilipili ambazo ni, pilipili mbuzi,mtama na kichaa,aina hizo hutofautiana kwa harufu na muonekeno.

Lakini pilipili ni tiba muhimu kwa binandamu kwani zinatumika kama malighafi muhimu kwenye bidhaa za viwandani, kwa wale waliowahi kukumbwa na zahma ya moshi wa mabomu ya machozi hufyatuliwa na askari polisi  pindi ghasia zitokeapo, basi fahamu kuwa pilipili zimetumika kama kiungo muhimu kutengeneza mabomu hayo.

Pilipili ina vitamin A,C, na K ambapo husaidia mfumo wa kinga dhidi ya magonjwa ya saratani na moyo kuimarisha ngozi ukuzaji nywele huku zikiwa na kemikali zinazotumika kushikilia seli pamoja mwilini,pia inasadia mwili kufyonza madini ya chuma,kuponya vidonda na  kuimarisha utendaji kazi wa ubongo.

Muhimu zaidi ni kwamba kemikali za pilipili husaidia seli nyeupe mwilini ambayo husaidia kwenye mfumo wa kinga mwilini,wataalamu wa afya nchini marekaniwalibainisha kuwa pilipili husaidia kupunguza uwezekano wa kupata  saratani ya mdomo, kongosho, tezi dume na tatizo la mmeng’enyo wa chakula.

Mtafiti wa masuala ya Afya na tiba, Jane Higdon,kutoka chuo kikuu cha Oregon state nchini marekani, anasema  kemikali za pilipili zinasaidia kuondoa sumu ambayo zinaharibu mfumo wa vinasaba (DNA), kuimarisha mifupa.kwa wavutaji wa sigara wanashauriwa kutumia pilipili kwenye milo yao ili hususani pilipili nyekundu kusaidia kupunguza sumu mwilini.

Pilipili pia husaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti kwa insulin kwa asilimia 60baada ya kula chakula , kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi.husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja mwilini ,kufungua kwa haraka na ufanisi pua zilzoziba kwa mafua na kukufanya upumue kwa urahisi,kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya utumbo, kuongeza kiwango cha kemikali ambayo husaidia kucchoma mafuta.

Pilipili manga husaidia  hasa kwa wanawake waliojifungua kutoa uchafu ambao umebakia kwenye kizazi, kupunguza maumivu ya tumbo na pia kushika mimba katika kipindi hicho hicho wakati unanyonyesha.

Ulaji wa pilipili unaweza kuwasaidia watu wanene au wanao ugua ugonjwa wa kisukari, hii ni kwa mujibu wa timu ya watafiti katika chuo kikuu cha Tasmania nchini Australia kupitia utafiti uliochapishwa katika American Journal of Clinical Nutrition, julai mwaka 2006.

Ili kupata faida za pilipili hakikisha mlo wakounakuwa na pilipili kwa kiwango, hakikisha unatumia pilipili halisi na siyo ya kueka kwenye makopo.upo uwezekano wa pilipili kuua na kutokomeza viini , endapo italiwa chini ya usimamizi na maelekezo ya Daktari.

Pilipili ikiwekwa kwa wingi kwenye chakula husababisha kuharisha hii itamfanya mtumiaji kupungukiwa na maji mwilini pamoja na kukosa nguvu,kwa mwanamke ambaye hana motto kupunguza matumizi ya pilipili kwan kwa kiasi kikubwa baadhi ya vyakula vyenye pilipili husababisha kutokushika ujauzito na vidonda vya tumbo.

Pia mlaji wa pilipili asitumie kiungo hicho kutibu kifua kwani akitumia anaweza kusababisha kukohoa kwa muda mrefu hadi kutoka damu kutokana na muwasho unao kwangua  kooni.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s