UGONJWA WA MTOTO WA JICHO (CATARACT)

JENNY CHILLERY NA FLORA HARRISON

Ugonjwa wa mtoto wa jicho ni ugonjwa unaongoza kwa upofu duniani, na watu wenye ugonjwa  huu mara nyingi huwa ni wazee na watoto.ugonjwa huu unatibikaendapo mwathirika wa tatizo hili atawahi mapema matibabu.

Ugonjwa huu mtu hupata ukungu kwenye jicho na kufanya kupunguza uwezo wake wa kuona au kutokuona kabisa,ukungu huo usambaa kwenye ile lenzi ya jicho na  kueka weupe kwenye macho.lakini pia ukungu huo hutofautiana kulingana na kasi ya motto wa jicho, wengine ukungu uonekana ata mtu akiwa mbali na wengine huonekana kwa kiasi kidogo sana kwenye jicho.

 

CHANZO CHA MTOTO WA JICHO

Inasababishwa na kujikuna macho muda mrefu ambayo mtu hujikuna na kuua lenzi ya jicho, kupigwa ngumi kwenye jicho na kuathiri lenzi ya jicho,j kwa wazee hutokana na uwezo wao wa kuona kupungua kwasababu ya uzee,kuumia sehemu ya jicho pia kunaweza sababisha mototo wa jicho na kukaa juani muda mrefu au kukaa sehemu yenye mwanga mkali na sababau nyingine ni mzio (allergy) ya vumbi ambayo hupelekea mtu kutoa vumbi kwenye macho kila wakati,  ana ajali.

 

DALILI ZA MTOTO WA JICHO

Huanza kwa kutoa ukungu mweupe katikati ya jicho,na pia humfanya mtu kushindwa kuona vizuri,  kuumia macho ata kwenye sehemu yenye mwanga mdogo,kushindwa kuona kabisa kwa ghafla.

Pia ugonjwa huu unapotokea mara nyingi huuathiri jicho moja , kwa wazee mara nyingi huathiri macho yote kwa wakati mmoja.

 

MAAMBUKIZI YA MTOTO WA JICHO

Ugonjwa huu hauambuzi kabisa.

TIBA YA MTOTO WA JICHO

Mtoto wa jicho tiba yake ni upasuaji mdogo ambao kwa kawaida  huchukua dakika 10 hadi 15 tu, na mgonjwa hutolewa ile lenzi iliyoshambuliwa na motto wa jicho kisha wataalamu wanaweka lenzi mpya itakayo msaidia mgonjwa kurudisha uwezo wake wa kuona,lakini pia ata baada ya upasuaji mgonjwa akishidwa kuona vizuri hupatiwa usaidizi wa miwani ili iweze kumuwezesha kuona vyema.

Mgonjwa anapowahi matibabu ni rahisi kurudisha uwezo wake wa kuona kama zamani lakin mgonjwa anapochelewa kupatiwa matibabu anaweza kusababisha kupata matatizo mengine ndani ya jicho ikiwemo saratani.

Baada ya matibabu mgonjw hapaswi kuinama muda mrefu au kukaa juani kwa muda mrefu au kupaka sabuni kwenye maeneo ya macho hadi hapo kidonda kitakapo pona kabisa kama ata kavyo elekezwa na Daktari.

Mototo wa jicho inatibika na kwa mkoa wa Dar es salaam Hospitali ya CCBRT ,Muhimbili na baadhi ya  hospitali wanatoa huduma izo za  matibabu. Mtu unapoona dadlili za ugonjwa huu ni vyema ukwahi hospitali kwa uchunguzi zaidi.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s