ZIJUE TIBA ZA ASILI NA NJIA ASILIA ZA KUTUNZA AFYA YAKO

 

Na Judith Geofrey (TUDARCo),

Matunda, mizizi na mboga mboga ni utajiri wa asili tuliopewa wanadamu. Katika vitu hivi utapata tiba asilia pamoja na viini lishe vyote vinavyohitajika na mwili kwa ajili ya afya yako Hapo kale tiba za asili zilionekana kama viini macho na uchawi, ila kwa uhalisia matunda, mizizi na mboga mboga ndiyo msingi haswa wa afya bora,katu ni tiba isiyo na uchoyo pia ni tiba isiyo na gharama.

Mtindo wa maisha unapokuwa mbaya huharibu afya kabisa lakini njia za asili za utunzaji afya, yaani tiba za asili, ni suluhisho kwa tatizo hilo. Ni matunda na mboga  hasa tutumiayo kila siku yaani Chungwa, Tufaha, Embe Ndizi, Sukuma wiki, Kabichi, mkunungu na mengineyo mingi ndiyo hasa chimbuko na kiini cha lishe bora.

Katika safu hii tutajifunza kwa undani namna matunda mboga mboga na mizizi ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa katika kutunza afya na kuhifadhi muonekano mzuri.

Leo tutaona tiba ya asili (mtindo wa maisha)kwa mgonjwa wa aina yoyote aliekosa lishe yaani unyafuzi (kwashiorkor) kuanzia aamkapo hadi mda wa kulala.

Saa 12:00 asubuhi

Ukiamka alfajiri kunywa ,

Chukua unga wa mkaa vijiko viwili vikubwa kisha changanya na maji ya uvugu vugu ukoroge kisha unywe ili kuondoa sumu zote katika mwili, kisha ongeza maji ya vugu vugu kwenye glasi kisha unywe.

Baada ya lisaa kunywa bilauri moja yenye mchanganyiko huu,

 • Karoti 2
 • Kitunguu maji kimoja saizi ya kati
 • Nyanya mbili
 • Punje mbili za kitunguu swaumu
 • Kabichi saizi ya kati robo
 • Na mboga ya majani yoyote utakayoipenda

Kisha kunywa uji wenye mchanganyiko wa nafaka nusu bilauri mfano uwele, ngano, ulezi, mahindi hasa ya njano.

Baada ya dakika kumi tumia kifungua kinywa chenye mchanganyiko huu,

 • Wanga (carbohydrate), mikate isiyotiwa chachu (isisyo na hamira), mihigo, viazi, chakula cha mchanganyiko wa mahindi na maharage, au chapatti, pia kuna aina za nafaka ambazo waweza kuchagua kwazo.
 • Maharage yaliyopikwa (maharage machanga) almaarufu kama “green beans”
 • Mchanganyiko wa mboga mboga kwa aina zake
 • Mwisho umalizie na bakuli la kachumbari

Baada ya masaa mawili kunywa kuanzia bilauri mbili za maji. Ifikapo saa 6:30 mchana kunywa bilauri moja ya maji ya uvugu vugu

Ifikapo saa 7:00 mchana kunywa bilauri moja ya mchanganyiko wa matunda yasiyopungua aina 5 mfano  (a) nanasi

(b) papai

(c) machungwa

(d) limao

(e) zabibu

Kisha kunywa bilauri moja ya uji wenye mchanganyiko wa nafaka.

Baada ya dakika kumi kula chakula cha mchana chenye wanga (kama ilivyokuwa kwenye kifungua kinywa) na mbegu (nuts) mfano karanga, korosho na nyinginezo kisha malizia kwa bakuli la kachumbari.

Baada ya masaa mawili kunywa bilauri mbili za maji ya uvugu vugu

Baada ya lisaa tena kunywa tena bilauri moja ya maji ya uvugu vugu.

Baada ya saa moja tena kunywa juisi ya matunda, nusu bilauri ya uji, ikifuatiwa na sahani ya kachumbari.

N.B

 1. Ni muhimu kachumbari (salad) ikachanganywa na vitunguu swaumu ili kuzuia minyoo
 2. Mgonjwa hapaswi kula baada ya saa 12:30 jioni na aachwe alale ifikapo saa 3:30 usiku
 3. Tiba hii ni ya kawaida ya magonjwa ya aina zote, japo yaweza kubadilika kutokana na maelekezo ya tiba ya ugonjwa husika, pia yaweza tumiwa hata na asiye mgonjwa.
 4. Pia hii sio mbadala wa dawa za mgonjwa (yaani dawa za kisasa hazihusiani na tiba hii, mgonjwa anaweza tumia tiba zote).

Toleo lijalo tutaona umuhimu wa tufaha (apple) na faida zake ni vipi ni tiba kwa mwili na afya inatibu magonjwa yapi.

Advertisements

2 Comments Add yours

 1. Asante mtaalam maana kuna ndugu yangu ana kwashiakor, nadhani hii ratiba inaweza kumsadiia

  Like

  1. mille abdul says:

   bila shaka robin jitahidi kuizingatia

   Liked by 1 person

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s