Umuhimu wa Kuyafahamu Madhara ya FISTULA na Tiba yake

Na Hidaya Nyanga

May, 23 ya kila mwaka ulimwengu unaadhimisha siku ya kimataifa ya mapambano dhidi ya tatizo la fistula ya uzazi kwa wanake. Kwa mwaka huu kauli mbiu inasema ‘Tumaini Uponyaji na Heshima kwa Mwanamke’.

Fistula ni miongoni mwa Tatizo ambalo limekuwa likawasumbua wanawake wengi katika jamii. Kitaalamu fistula ni tundu linavujisha vitu katika njia ya uzazi inaweza ikawa ni mkojo (Vesco Vaginal Fistula), haja kubwa (Rectal Vaginl Fistula) au vyote kwa pamoja.

 

Kwa mujibu wa Shrika la afya dunian (WHO) tatizo la fistula lipo zaidi katika bara la Asia, Amerika Kusini na Afrika hususani nchi zilizopo kusini mwa jangwa la sahara kwani tatizo hilo lipo Zaidi katika maitafa masikini kiuchumi.

Duniani wanawake milioni mbili wanakadiliwa kuishi na fistula na wanaotubiwa ni 20,000 tu. Kila mwaka wagonjwa wapya wanaopatikana ni 50,000 hadi 100,000 jambo ambalo linaonyesha kuwa kuna wagonjwa wengi wanendelee kupatikana huku wengine wakiwa hawajatibiwa.

Afrika mashariki kila mwaka Tanzania inakuwa na wanawake wenye tatizo la fistula 3,000, Kenya 3,000, Uganda 1900, Burundi 1000- 2000, Rwanda 415.

Kwa Tanzania wanawake wenye tatizo la fistula 1,500 hadi 2,000 hupatiwa matibabu na wengine hawapati fursa hiyo kutokana na uchache wa wataalamu, umasikini na ufahamu mdogo juu ya tatizo hili.

Mkurugenzi mkazi wa Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na idadi ya watu (UNFPA), anasema Utashi wa kisiasa na uwekezaji katika sekta ya afya nchini ni mambo ambayo yanatakiwa kufanyika Ili kumaliza tatizo la ugonjwa wa Fistula ambao umekuwa ukiwasumbua maelfu ya wanawake nchini.

“Nchini Tanzania wanawake zaidi 3,000 wanaugua ugonjwa wa fistula na wengi hawajapatiwa matibabu kwasababu ya kukosa elimu na maarifa juu ya ugonjwa huo, upungufu wa watalaam, vifaa tiba na umasikini ambao husababisha wagonjwa kukosa fursa ya kupata matibabu,” anasema Dk Begum.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Upasuaji wa Fistula katika Hospitali ya CCBRT, Dk. James Chapa anasema ya zaidi ya asilimia 90 ya wanawake wanaopata tatizo hilo hutokana na uchungu pingamizi ambao husababisha mtoto kushindwa kutoka wakati wa uchungu.

Uchungu pingamizi unaweza kutokana na ukubwa mtoto usiolingana na nyonga ya mzazi. Mtoto anakwama lakini tumbo la uzazi linaendelea kusukuma mpaka mtoto atoke suala ambalo husababisha majeraha kwakuwa mtoto huendelea kukandamiza kibofu na njia ya haja kubwa.

“Nyonga ya mama inaweza ikawa ndogo kwakuwa hakupata lishe nzuri wakati wa udogo au auliugua utapiamlo lakini pia mama anaweza akawa aliwahi kupata ajali ambayo ilimsababishia matatizo katika nyonga zake, ”anasema Dk Chapa.

Mbali na sababu hiyo tatizo la fistula pia linasababishwa na upasuaji ambapo daktari anaweza kutia jeraha kwenye kibofu cha mkojo wakati akifanya matibabu ya tatizo jingine.

“Kwa tukio ambalo hatulipendi, Fistula ambazo zinasababishwa na upasuaji zinaendelea kuongezeka, Tatizo huenda lipo kwenye ufundishaji wa madaktari wetu au amama alifika hospitali kwa kuchelewa,”anasema Dk Chapa.

Anasema fistula imekuwa ikichangiwa na familia kuchelewa kuamua kumpeleka hospitali mama mjamzito, ucheleweshaji wa miundoninu familia imejipanga lakini usafiri hakuna au barabara hazipitiki na ucheleweshaji katika kituo cha afya (mama amefika lakini hakuna mkunga mtaalamu na vifaa tiba).

“Mapambano ya fistula yanakwma kwasababu stula yapo chini kwasababu madaktari wanaofanya upasuaji bado ni wa wachache kwa nchinzima wapo 16 pekee na wengine sasa hawafanya huduma wapo katika vitengo vingine. Tukitegemee kutibu tu hatuwezi kuwafikia wagonjwa wote hivyo basi tunatakiwa kuwekeza katika kinga Zaidi na kumaliza changamoto ya uhaba wa vifaa tiba,”anasema Dk Chapa.

Hata Meneja wa programu ya afya ya uzazi, mama na mtoto wa Shirika la umoja wa matifa linaloshughulika na Idadi ya watu (UNFPA), Felister Bwana anasema ugonjwa wa fistula unauhusianao na changamoto za afya uzazi hivyo mapambano yake ni lazima yaanzie kwa kuongeza wataalamu wa afya ya uzazi.

“Fistuli inasababishwa na uzazi pingamizi na inawezekana kuzuilika, endapo mama mjamzito atahudumiwa na daktari ama mkungu mwenye ujuzi kwakuwa huduma zozote za kitabibu zitayohitaji kwa mama mjamzito kabla na baada ya kujifungua zitapatikana,”alisema Bwana.

Bwana anasema ili kutokomeza tatizo la fistula kwa wanawake nchini Serikali inapaswa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya tatizo hili sanjali na kuhakikisha inamaliza changamoto ya upungufu wa watumishi wa afya wenye ujuzi stahiki katika vituo vyote nchini.

Wasemavyo waathirika.

Ushuhudu unaotolewa na baadhi ya waathirika unaonyesha kuwa mapambano ya ugonjwa wa Fistula yanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa elimu na na maalifa, wakunga wenye utaalamu na madaktari bingwa wa ugonjwa huo.

Mastidia Jacob Mkazi wa Wilaya ya Mleba Mkoani Kagera ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya CCBRT anasema  alipata ugonjwa wa fistula mwaka 2006 wakati niposhikwa na uchungu wa kujifungua.

Nilipelekwa hospitali nikaambiwa nisubiri nijifungue lakini baada ya kusubiri kwa muda mrefu nikaelezwa kuwa haiwezekani tena kujifungua kwakuwa mtoto alikuwa amekwishafariki hivyo nitafanyiwa upasuaji,”anasema Mastidia.

Anasema baada ya kufanyiwa upasuaji aliwekewa mpira wa mkojo ambao alikaa nao kwa siku saba na ulipotolewa alanza kutokwa na mkojo bila kujizuia, Aliwaeleza wahudumu wa hospitali juu ya tatizo hilo lakini wakamtaka ajaribu kubana misuli kwa madai kuwa huenda ililegea.

Mastidia anaongeza kuwa baada ya kutakiwa kujaribu kubana misuli aliruhusiwa kwenda nyumbani lakini tatizo hilo liliendelea na aliporudi hospitali kwa mara nyingine aliambiwa kuwa tatizo hilo hawawezi kulitibu na badala yake aende Hospitali ya rufaa Bugando au asubili wataalamu watakapokuja kutoa huduma katika hospitali hiyo.

“Wakati naambiwa kusubiri wataalamu hao ilikuwa ni mwezi watano na wao walitarajiwa kufika katika hospitali hiyo mwezi wa kumi. Ilinibidi nirudi nyumbani kutafta pesa kwaajili ya kwenda Bugando lakini baadaye nilipata taarifa za CCBRT kupitia vyombo vya habari. Nikaja huku kwaajili ya matibabu, sasa nimepona nasubiri kuruhusiwa,”alisema Mastidia.

Mwingine ni Sukujua Mabula (19) ambaye alishikwa na ugonjwa huo mwaka jana baada ya kupatwa na uchungu pingamizi uliosababishwa na ukubwa wa mtoto na ufinyu wa nyonga zake.

Lakini tatizo hilo kwa kiasi kikubwa liliasababishwa na ufahamu mdogo wa familia kwani madaktari walimueleza tangu awali kuwa hataweza kujifungua kwa njia ya kawaida pasipo upasuaji lakini wakwe zake walimueleza asithubutu kukubali kufanyiwa upasuaji kwakuwa anaweza kupoteza maisha yake nay a mtoto wake.

“Nilpoanza kushikwa na uchungu nilimwambia mamamkwe lakini akaniambia nisiende hospitali nitajifungulia nyumbani hapo kwakuwa watoto wake wote amewazalisha mwenyewe na kuchelewa huko kujifungua ni kwasababu nilichanganya wanaume wakati sio kweli,”anasema Sikujua.

Anasema mamkwe wake alijaribu kumzalisha lakini ilishindikana baada ya mtoto kutoka kichwa tu ndipo akapelekwa hospitali na alipofika mtoto alikuwa tayari alikuwa ameshafariki hivyo manesi wakamsaidi kumtoa.

“Baada ya mtoto kutolewa nilikaa katika hali ya kutojitambu kwa siku nzima na baadaye nilizinduka lakini nilikuwa siwezi kutembea na tayari haja kubwa na dogo zilikuwa zinanitoka bila kujizuia,”anasema Sikujua.

Hali hiyo iliendelea kwa Sikujua na hakujua kama tatizo lake lilikuwa ni fistula ya uzazi mpaka pale aliposikia matangazo katika vyombo vya habari, “Baada ya kusikia taarifa katika vyombo vya habari nilifika katika ofisi wa wakala wa CCBRT ndiye akanifanyia taratibu za kuja huku kuanza matibabu”.

Madhara yatokanayo na Fistula

Baada ya mtu kupata tatizo na fistula anaweza kupata matatizo ya kiafya, kijamii na kiuchumi.

Kiafya mwanamke mwenye fistula hutokwa na haja kubwa na ndogo inayokuwa na harufu kali muda wote, kuugua vidonda sehemu za siri, mawe ukeni au kwenye kibofu cha mkojo, kupoteza uwezo wa kuzaa na kutoweza kushiriki tendola ndoa.

Kijamii mtu mwenye fistula hunyanyapaliwa katika jamii, kutelekezwa na mwenza wake kutokana na hali yake ya kimwili, kutengwa na kushindwa kushiriki shughuli za kijamii, aibu na kutojiamini na msongo wa mawazo kwasababu wakina mama wengi wenye fistula hupata mtoto mfu.

Pia kiuchumi mwanamke mwenye fistula huishia kuishi maisha ya dhiki na kuporomoka kiuchumi kwakuwa hawezi tena kushiriki shughuli za uzalishaji mali kama awali.

Kinga ya Fistula.

Kama ilivyokawaida kinga nio bora kuliko tiba Dk anasema ili kujikinga na tatizo la fistula ni mama mjamzito kuwahi kwenda kujifungulia kwenye kituo cha kutolea huduma za afya na Serikali kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya ya uzazi.

Pia Daktari anasema jamii ni mhimu ikawa na elimu ya hali halisi ya tatizo pamoja na wazazi kuwapatia lishe nzuri watoto imbayo inatawasaidia kukua vizuri ili wasikumbane na tatizo la kutotanuka kwa nyonga zao.

Matibabu ya Fistula.

Dk .. anasema matibabu ya Fistula ni kufanya upasuaji na kuziba sehemu ya tundu linalokuwa limetokea ambapo baada ya upasuaji mama aliyefanyiwa upasuaji anakaa siku 14 akiwa anatumia mpira kutoa haja na baada ya hapo anakuwa amepona vizuri.

Hospitali ambazo zinatibu tatizo la fistula nchini ni CCBRT ya Dar Es Salaam, Bugando Mwanza, Selain Arusha, Nkinga Tabora, St Joseph Peramiho, KCMC, Moshi, Kabanga Kigoma, Hospitali ya mkoa wa Lindi, Ruvuma, Dodoma, Morogoro, Kigoma na Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s