Jinsi ya Kutunza Ngozi Yenye Mafuta

Na: Anna Lukele

Kuna aina mbili za ngozi.  Ngozi kavu na Ile yenye mafuta ambayo Mara nyingi hupelekea chunusi katika sehemu mablimbali za mwili hasa usoni, kifuani na mgongoni . Watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na changamoto ya chunusi inayosababishwa na ngozi kuwa na mafuta mengi jambo ambalo hupelekea kutokujiamini hasa wakiwa mbele za watu na hata kushindwa kwenda kwenye baadhi ya mitoko kutokana na nyuso zao kuwa na chunusi nyingi

 

 

Hizi ndio njia bora, za kiasili na zisizo na madhara wala gharama zitakazo kuwezesha kutunza ngozi yenye mafuta.

 

Epuka kula kwa wingi vitu vyenye mafuta,  mfano karanga, korosho , ufuta au vyakula vilivotiwa mafuta mengi. Hiyo itakusaidia kupunguza wingi wa mafuta katika mwili.

 

Usioshe uso wako, au mwili kwa ujumla kwa kutumia sabuni zenye kemikali . Kwa kufanya hivi utafanya ngozi yako kuharibiwa na kemikali zilizoko kwenye sabuni.

 

Pendelea kuosha uso wako kwa maji ya moto Ili kufanya mafuta yasigandiane katika mwili wako.

 

Osha uso au ngozi yako kwa ujumla walau Mara tatu kwa siku. Usipende kukaa muda mrefu bila kuosha ngozi yako. Hakikisha unalala uso ukiwa msafi .

 

Kuwa mwangalifu usikwaruze uso wako. Ukipata michubuko ngozi hutoa mafuta mengi Ili kuziba sehemu hizo zenye mikwaruzo.

 

Kunywa maji ya kutosha, walau lita tatu mpaka tano kwa siku.

 

Pendelea kufanya mazoezi. Mazoez ya mwili husaidia mafuta katika ngozi kuyeyuka na kutoka kwa njia ya jasho, pia husababisha matundu ya hewa katika ngozi kufunguka ambapo yakifunguka sio rahisi mafuta kirundikana na kutengeneza chunusi.

 

Kumbuka: mazoezi si lazima uende gym. Pendelea kutembea kwa mguu katika sehemu zisizo na ulazima kupanda gari, shughulisha mwili wako kwa shughuli za nyumbani Ili uweze kutoa jasho kwa wingi, lakini pia itakusaidia kupata hamu ya kunywa maji kwa wingi.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s